Hip hop

From Wikipedia, the free encyclopedia

Hip hop
Remove ads

Hip hop ni aina ya muziki unaoelezea aina ya usanii na utamaduni uliyotokana na jamii ya Wamarekani Weusi na Walatino kunako miaka ya 1970 mjini New York City, hasa katika kitongoji cha Bronx.[1][2][3]

Thumb
Ma DJ wa muziki wa Hiphop wakitengeneza muziki

DJ Afrika Bambaataa alieleza kwa muhtasari wa nguzo nne za utamaduni wa Hip hop: U-MC, U-DJ, breaking na uandikaji wa graffiti.[4][5][6]

Elementi nyingine ni pamoja na beatboxing.[7]

Remove ads

Uenezi

Kwa vile imeibukia kutoka mjini South Bronx, utamaduni wa Hip hop umeenea dunia nzima.[8]

Muziki wa hip hop awali ulianzishwa na Ma-DJ waliokuwa wanatengeneza midundo kwa kutumia mtindo wa kurudirudia na kusimama (hasa katika visehemu vidogo vya muziki wa kusisitiza mwelekeo wa kigongoma) kwenye turntable mbili, hasa hujulikana kama kusampo muziki.

Hii baadaye ikaja kusindikizwa na "rap", mtindo wa wizani unaotoa maneno au mashairi yaliyo kwenye vipimo vya mstari ulalo wa nota 16 katika fremu ya muda, ikiwa sambamba na beatboxing, maujanja ya sauti hutumika hasa katika kugezea mfumo wa midundo na elementi za muziki mbalimbali na mautundu na vionjo kadhaa kutoka kwa Ma-DJ wa hip hop.

Muundo kamili wa kudansi na staili kadha wa kadha za mavazi zimezua mashabiki miongoni mwao katika muziki mpya. Elementi hizi zimeonesha mabadiliko ya na maendeleo kadha wa kadha katika historia ya utamaduni huu. Baadhi ya miziki ya hip-Hop hutoa maelezo ya kisiasa.

Mahusiano baina ya graffiti na utamaduni wa hip hop unatokana mionekano mipya tofauti iliyoongeza ufafanuzi wa kina na uenezi tofauti wa kivitendo ambapo kwingine walichukulia elementi ya hip hop kama sehemu ya sanaa, kukiwa na mpitilizo mkubwa baina ya hao wanaondika graffiti na hao wanaotenda elementi zingine za hip hop kivyao. Leo hii, graffiti imebakiwa kuwa sehemu ya hip hop, wakati kwa upande wa sanaa imechukua eneo kubwa katika masuala ya picha na michoro katika maeneosho mbalimbali duniani kote.

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Tazama pia

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads