Uongofu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Uongofu (pia: Wongofu, kutoka kitenzi kuongoa) ni tendo la hiari la mtu la kubadilika upande wa dini au wa madhehebu, lakini pia upande wa maadili ili kuishi vizuri zaidi[1][2]. Uamuzi huo unaleta matokeo mengi, pengine makubwa katika maisha ya mhusika na jamii yake. Si wote wanafurahia uamuzi huo, hivyo pengine mtu atapatwa na dhuluma za namna mbalimbali.

Tamko la kimataifa la haki za binadamu (n. 18) linasema: «Kila mmoja ana haki ya kuwa huru katika kuwaza, kufuata dhamiri yake na dini; haki hiyo inajumlisha haki ya kubadili dini au imani, na uhuru katika kujulisha, peke yake au pamoja na wengine, hadharani na katika mahusiano binafsi, dini yake au imani yake katika kufundisha, kutenda, kuabudu na kushika taratibu za ibada.»[3][4]
Pengine tendo la kubadilika linatazamwa upande hasi na kuitwa uasi na watu wa dini au madhehebu ambayo mhusika ameachana nayo.
Vilevile juhudi za kuongoa watu kama umisionari zinaweza kutazamwa upande hasi na kupingwa hata na sheria au serikali.
Ndiyo sababu mara nyingine ni vigumu kutekeleza vizuri hiyo haki ya binadamu.
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads