Zoe Saldana
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Zoé Yadira Zaldaña Nazario[1][3] (anafahamika zaidi kama Zoe Saldana, wakati mwingine huandikwa Zoë[4]; amezaliwa 19 Juni 1978) ni mwigizaji wa filamu kutoka nchini Marekani. Alipata uhusika wake katika filamu ya mwaka wa 2000 Center Stage, na baadaye kupata umaarufu zaidi kwa uhusika wa Anamaria kwenye Pirates of the Caribbean: Curse of the Black Pearl, Uhura kwenye filamu ya mwaka wa 2009 Star Trek, na Neytiri kwenye filamu ya James Cameron Avatar. Mwaka wa 2010, ameonekana kwenye filamu ya The Losers na Takers.
Remove ads
Maisha ya awali
Saldana alizaliwa kama Zoé Yadira Zaldaña Nazario huko mjini Passaic, New Jersey,[2][5] Marekani, na Aridio Zaldaña, Mdominika, na Asalia Nazario, M-Puerto Rika.[6][7][8][9]
Lugha yake ya kwanza ni Kiingereza na Kihispania. Ametumia utotoni mwake akikulia huko mjini Queens, New York. Akiwa na umri 10, alihamia Jamhuri ya Dominika, ambapo waliishi kwa miaka mingine saba. Saldana amejiunga katika darasa la ballet katika moja kati ya shule za dansi za majigambo katika Jamhuri ya Dominika. Baada ya kurudi mjini Queens akiwa na umri wa 17, akaanza kutumbuiza kikindi cha kibisa cha Faces, ambacho kinachohusisha na michezo ya kusambaza ujumbe wa kheri kwa vijana, kupitia mandhari yanayohusiana na masuala ya utumiaji wa dawa za kulevya na ngono kwa ujumla. Michezo hiyo haikumpa uzoefu wa haja tu bali ilikuwa chanzo cha majivuno na sifa kubwa kwake, pindi alipogundua ya kwamba analeta mabadiliko katika maisha ya vijana wa lika lake. Wakati anatumbuiza na kikundi cha kibisa cha Faces na pia New York Youth Theater Zoe akachaguliwa na wakala wa vipaji. Mafunzo yake ya dansi katika miaka ya awali, jumosha na uzoefu wake wa uigizaji, kumemsaidia vilivyo kuwekza kucheza vyema uhusika wake wa kwenye skrini kubwa akiwa kama Eva, akiwa kama mcheza ballet mwenye kipaji na ushapavu katika filamu ya mwaka wa 2000 Center Stage.
Tar. 30 Juni 2010, imetangazwa kwenye Us Weekly kwamba Saldana amevishwa pete na bwana wake wa miaka 10, mwigizaji na CEO wa My Fashion Database Keith Britton.[10]
Remove ads
Filmografia
Remove ads
Marejeo
Viungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads