Zoltán Trepák
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Zoltán Trepák (amezaliwa tar. 20 Februari 1977 mjini Budapest, Hungaria) ni mchezaji mpira wa kikapu wa kulipwa kutoka nchini Hungaria.[1]

Remove ads
Shughuli
Alianza kucheza mpira wa kikapu huko mjini Csepel, lakini baada ya mwaka mmoja ile timu aliokuwa akichezea ikatoweka katika uwanja wa michezo, na akelekea katika timu ya Falco KC ambayo ipo mjini Szombathely. Akiwa kule alitumia miaka mitatu, kisha baadaye akaja kuchezea miaka mitatu kule mjini Szolnok.
Miaka kadhaa baadaye akaingia mkataba na Kaposvár kwa muda wa miaka mitatu. Akiwa bado anaichezea Szolnok, akabahatika kuichezea timu ya taifa, mnamo 2001. Baada ya miaka sita, akacheza tena kule, na sasa ni mchezaji aliyeichezea timu ya taifa kwa mara zipatazo 15.
Baada ya Kaposvár akacheza katika Nyíregyháza, kati ya 2006 na 2008, mnamo 2008 alienda zake Zalaegerszeg.
Tarehe 10 Januari 2008, amecheza mechi yake kali kati ya Waslovakia na Spišská Nová Ves, amepata pointi 28[1][2]
Klabu zake
- 1995-1996 - Csepel
- 1996-1999 - Falco KC (Szombathely)
- 1999-2003 - Szolnoki Olaj KK (Szolnok)
- 2003-2006 - Kaposvári KK (Kaposvár)
- 2006-2008 - Marso-Vagép NYKK (Nyíregyháza)
- 2008- - Zalakerámia ZTE KK (Zalaegerszeg)
Remove ads
Marejeo
Viungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads