Mtini ni mti mkubwa, kama kichaka au mdogo wenye asili ya kusini magharibi mwa Asia na pande za mashariki mwa Mediteranea. Huwa na kimo cha mita 6.9 mpaka 10, na shina laini la kijivu. Majani yana urefu wa sm 12-15 kwa urefu na sm 10 -18 kwa upana, yakiwa yamegawanyika katika vipande vitatu au vitano. Matunda yake, matini huwa na urefu wa sm 3-5 na ngozi ya kijani, wakati mwingine huwa na kuwa ya zambarau au kahawia. Majimaji ya tini huwasha ngozi ya binadamu.
Mtindo wa Kigothi katika usanifu majengo wa Ulaya ni mtindo ulioanza katika karne ya 12 na kutumika hadi mnamo 1500. Mtindo huo ulichukua nafasi ya mtindo wa Kiroma uliotumika kabla yake. Ulionekana pia katika matawi mengine ya sanaa. Katika karne ya 19 ulitumika upya kwa majengo makubwa katika mtindo wa Kigothi mamboleo.