Mtipitipi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mtipitipi (pia mturituri, mchechepwa, kikwajuzi, kitimutimu, sindamu na songu; kwa lugha ya kisayansi Abrus precatorius) ni mmea mtambaa wa familia Fabaceae. Mbegu zake nyekundu na nyeusi huitwa matipitipi na hutumika kama shanga.
Matipitipi yana sumu ndani yao inayoitwa abrini na iliyo na mnasaba na risini, sumu ya mbegu za mbarika. Ganda la mbegu ni gumu sana. Kwa hivyo kumeza tipitipi lisilovunjika hakuleti shida, kwa sababu mbegu inanyewa bila badiliko. Lakini kutafuna na kumeza tipitipi moja tu kunaweza kumwua mtu mzima. Udungaji wa kiasi kidogo cha abrini unamwua mtu pia. Kwa hivyo kutoboa matipitipi na kuyatumia kama shanga ni hatari sana.
Remove ads
Picha
- Majani
- Kishada cha maua
- Matumba, moja likionyesha matipitipi
- Matipitipi
- Ukoja wa matipitipi
![]() |
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mtipitipi kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Remove ads
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads