Vanua Lava ni kisiwa cha Vanuatu, kimojawapo cha Visiwa vya Banks. Kiko upande wa kaskazini wa kisiwa cha Gaua. Eneo la kisiwa ni 314 km². Mji mkubwa kabisa kisiwani huitwa Sola. Mwaka wa 2009 idadi ya watu kisiwani imehesabiwa kuwa 2623. Watu wakaao kisiwani kwa Vanua Lava huongea hasa Kivures na Kivera'a.