Ataindum Donald Nge ni mwanamuziki wa Kameruni na mtumbuizaji anayefahimika kwa jina la Ibali akiwa jukwaani. Pia ni mwanaharakati wa haki za binadamu.
Ibiolola Amao ni mhandisi, mshauri mkuu wa Huduma za Lonadek kati ya Uingereza na Nigeria. Alikuwa ni mshauri katika mipango mbalimbali mnamo mwaka 2020 nchini Nigeria. Alipata tuzo mbalimbali kama vile, mfanyabiashara bora na mchapakazi wakike (IWEC) mnamo mwaka 2016, Energy Institute Champion mnamo mwaka 2016, C3E international woman of distinction Award, Access Bank “W” 100, Forbes Africa rising star Award mnamo mwaka 2019. Alikuwa mwanachama wa vital voices (vv) grow fellow, mwanachama wa vv100 wa kimataifa wa WEConnect. Ibiolola pia alikuwa mwanzilishi wa mradi wa mierezi pamoja kituo cha ujasiriamali.