Yohane Baptista de La Salle
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yohane Baptista de la Salle (kwa Kifaransa: Jean-Baptiste de La Salle; Reims, Ufaransa, 30 Aprili 1651 - Saint-Yon, Rouen, Ufaransa, 7 Aprili 1719) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mlezi wa vijana wengi, hasa fukara, ambaye kwa ajili ya malezi yao ya kiutu na ya Kikristo alianzisha pia kwa tabu nyingi shirika la Mabradha wa Shule za Kikristo. Anahesabiwa mwanzilishi wa shule Katoliki duniani. De La Salle anahesabiwa pia kuwa wa kwanza kuendesha chuo cha ualimu (1685).