Alipius wa Thagaste
From Wikipedia, the free encyclopedia
Alipius wa Thagaste alikuwa askofu wa Tagaste (leo nchini Algeria) mwaka 394. Inasemekana ndiye wa kwanza kujenga monasteri sehemu hiyo ya Afrika.
Baada ya kuwa mwanafunzi wa Augustino wa Hippo, akawa kwa muda mrefu sana rafiki yake akaungana naye katika kuongokea Kanisa Katoliki (386; Confessions 8.12.28), katika maisha ya kiroho na uchungaji, ikiwa ni pamoja na kupinga uzushi[2].
Karibu yote tunayoyajua juu yake yanatokana na kitabu cha Augustino juu ya maisha yake mwenyewe Maungamo (Confessiones).
Papa Gregori XIII alimtangaza mtakatifu mwaka 1584[3] .