Antoni wa Kiev
From Wikipedia, the free encyclopedia
Antoni wa Kiev au Antoni Pekerski (kwa Kirusi Антоний Печерский; kwa Kiukraina Антоній Печерський; Liubek, 983 hivi - Kiev, 7 Mei 1073) alikuwa mkaapweke kwenye mlima Athos (Ugiriki) hadi alipotumwa kurudi kwao kueneza umonaki katika sehemu za Kiev (leo nchini Ukraina) zilizopokea Ukristo tangu muda mfupi[1].
Baada ya kuanzisha monasteri kadhaa[2], alirudi upwekeni kwenye mlima Athos hadi alipotumwa tena Kiev ambapo, pamoja na Theodosi wa Kiev alianzisha ile maarufu ya Mapango ya Kiev.
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 7 Mei[3] lakini pia tarehe 23 Julai.