Antoni wa Mt. Ana
From Wikipedia, the free encyclopedia
Antoni wa Mt. Ana Galvão, O.F.M., kwa Kireno Antônio de Sant'Anna, maarufu nchini Brazil kama Frei (Ndugu) Galvão (Guaratinguetá, 1739–23 Desemba 1822) alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo wakati wa ukoloni.
Mmoja kati ya Wakristo wanaojulikana zaidi kati ya watu wa nchi yake, pia kutokana na miujiza iliyofanyika kwa njia yake,[1] Galvão alitangazwa mtakatifu na Papa Benedikto XVI tarehe 11 Mei 2007, akiwa wa kwanza kati ya wazawa wa Brazil.[2]
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake kila mwaka[3].