Gotardo wa Hildesheim
From Wikipedia, the free encyclopedia
Gotardo wa Hildesheim, O.S.B. (jina asili: Gotthard au Godehard; Niederaltaich, Bavaria, 960 – 4 Mei 1038) alikuwa mmonaki, padri, abati na hatimaye (2 Desemba 1022) askofu nchini Ujerumani[1].
Kama kiongozi wa wamonaki, alitembelea na kuanzisha monasteri mbalimbali. Halafu kama askofu alijitahidi kustawisha jimbo lake, akirudisha nidhamu kati ya wakleri na kuunda shule kadhaa.
Papa Innocent II alimtangaza mtakatifu mwaka 1131.
Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki na Waorthodoksi tarehe 5 Mei[2].