Jose Vaz
From Wikipedia, the free encyclopedia
Jose Vaz, CO, (kwa Kikonkani: Zuze Vaz; kwa Kireno: José Vaz; kwa Kitamil: புனித யோசப் வாஸ், Punidha Yosap Vaz; kwa Kisinhala: ශාන්ත ජුසේ වාස් මුනිතුමා, ශ්රී ලංකාවේ අපොස්තුළුවරයා, Santha Juse Vaz Munithuma, Sri Lankawe Aposthuluvaraya; Benaulim, Goa, India, 21 Aprili 1651 – Kandy, Sri Lanka, 16 Januari 1711) alikuwa padri wa Oratorio ya Mt. Filipo Neri, mmisionari nchini Sri Lanka.
Vaz alifika huko wakati kisiwa hicho kimetekwa na Waholanzi, ambao walitaka kulazimisha Ukalvini uwe dini rasmi . Bila kujali dhuluma yao, Jose aliizunguka nchi yote akiwapatia Ekaristi na sakramenti nyingine Wakatoliki waliobaki baada ya Wareno kufukuzwa. Kwa namna hiyo Vaz alidumisha Kanisa Katoliki nchini, hata akaitwa mtume wa Ceylon.
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 21 Januari 1995, halafu Papa Fransisko alimtangaza mtakatifu tarehe 14 Januari 2015.[1]