Kushukia kuzimu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kushukia kuzimu ni fundisho la imani ya madhehebu mbalimbali ya Ukristo la kwamba Yesu Kristo, baada ya kufa msalabani siku ya Ijumaa kuu na kabla ya kufufuka kwa utukufu usiku wa Pasaka, alishukia kuzimu kwa nguvu ili kutoa roho za waadilifu zilizokuwa zikisubiri ukombozi kutoka kwake.[1]
Msingi katika Biblia ya Kikristo ni hasa dondoo la Waraka wa kwanza wa Mtume Petro 3:18-22 na Waraka wa Mtume Paulo kwa Waefeso 4:9[2] This near-absence in Scripture has given rise to controversy and differing interpretations.[3].
Katika karne za kwanza za Kanisa, imani hiyo inakiriwa na Kanuni ya Imani ya Mitume (Italia) na Ungamo la Imani la Atanasi (Misri). Ilifundishwa pia na Melito wa Sardi, Tertuliani, Hipoliti wa Roma, Origen, Ambrosi n.k.