From Wikipedia, the free encyclopedia
Majira ya joto (pia: chaka; kwa Kiingereza Summer) ni mojawapo kati ya majira manne ya kanda za wastani, na halijoto yake ni ya joto kuliko majira mengine.
Inaweza kulinganishwa na chaka ambayo ni kipindi cha joto katika Afrika ya Mashariki.
Kadiri ya umbali na ikweta, mchana ni mrefu na usiku ni mfupi. Ndiyo sababu majira hayo yanaitwa ya joto.
Sehemu nyingine joto ni kali kiasi kwamba kwa miezi 2-3 shule huwa zimefungwa.
Yanafuata majira ya kuchipua (kwa Kiingereza "Spring") na kutangulia majira ya kupuputika majani (kwa Kiingereza "Fall" au "Autumn").
Majira hayo yanatokea duniani kwa nyakati tofauti kadiri eneo husika lilivyo kaskazini au kusini kwa ikweta. Hata katika nchi ileile, kwa mfano Kenya, majira ni tofauti upande huu na upande huu wa ikweta.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.