Wadudu mabawa-manyofu ni wadudu wadogo hadi wakubwa wa oda Orthoptera katika nusungeli Pterygota (wenye mabawa). Jina ni tafsiri ya jina la kisayansi. Wadudu hawa wanajulikana sana kama panzi, nzige, nyenje, chenene na senene k.m.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Mdudu mabawa-manyofu
Thumb
Panzi-vundo kijani (Phymateus viridipes)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Orthoptera (Wadudu wenye mabawa manyofu)
Latreille, 1793
Ngazi za chini

Nusuoda 2, familia za juu 15:

  • Caelifera (Panzi Vipapasio-vifupi) Ander, 1936
    • Acridoidea (Panzi-mbuga) Macleay, 1819
    • Eumastacoidea (Warukaji-mwitu, Panzi-kibiriti) Burr, 1899
    • Pneumoroidea (Panzi-kibofu) Blanchard, 1845
    • Pyrgomorphoidea (Panzi Rangirangi) Brunner-Von Wattenwyl, 1874
    • Tanaoceroidea (Panzi-jangwa vipapasio-virefu) Rehn, 1948
    • Tetrigoidea (Panzi vibete) Rambur, 1838
  • Ensifera (Panzi Vipapasio-virefu)
    • Grylloidea (Nyenje) Laicharting, 1781
    • Gryllotalpoidea (Chenene) Leach, 1815
    • Hagloidea Handlirsch, 1906
    • Rhaphidophoroidea (Nyenje-pango au weta-pango) Brunner-Von Wattenwyl]], 1888
    • Schizodactyloidea (Nyenje-matutamchanga)
    • Stenopelmatoidea (Weta, Nyenje-Jerusalemu) Burmeister, 1838
    • Tettigonioidea (Senene na jamaa) Krauss, 1902
  • Bila nusuoda
    • Tridactyloidea (Panzi wachimbaji) Brullé, 1835
    • Trigonopterygoidea (Panzi-jani) Walker, 1870
Funga

Mabawa ya mbele ya wadudu hawa ni magumu kiasi na kufunika yale ya nyuma yakiwa yamekunjwa juu ya fumbatio. Mabawa ya nyuma ni kama viwambo na mapana upande wa msingi. Kwa kawaida mabawa ni marefu kuliko fumbatio lakini mara nyingi yako mafupi, hata mafupi sana. Zaidi ya hayo spishi nyingi hazina mabawa yoyote.

Sehemu za kinywa zinafaa kutafuna na zinaweza kuwa kubwa na zenye nguvu. Hula nyasi na mimea yenye majani mapana kwa kawaida lakine spishi nyingi za Ensifera hula wadudu wadogo pia.

Tofauti kati ya nusuoda ni urefu wa vipapasio. Vile vya Caelifera ni vifupi kuliko mwili na vile vya Ensifera ni virefu kama mwili au kupita mwili. Pia majike wa Ensifera wana mrija mrefu wa kutaga ambao unaweza kuwa na umbo la upanga au la sindano. Wale wa Caelifera wana vali mbili za kutaga.

Spishi za Caelifera hutaga mayai katika ardhi kwa kawaida, pengine ndani ya mashina ya mimea. Nyingi za zile za Ensifera hutaga ndani ya tishu za mimea, lakini nyingine zinatage ardhini.

Spishi kadhaa za Afrika ya Mashariki

Caelifera

Ensifera

  • Gryllotalpa africana, Chenene
  • Gryllus bimaculatus, Nyenje Madoa-mawili
  • Ruspolia differens, Senene

Tridactyloidea

  • Afrotridactylus usambaricus, Chenene Kibete

Picha

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.