![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/9/9d/Facial_Chronicle_-_b.13%252C_p.443_-_Council_in_Trullo.gif/640px-Facial_Chronicle_-_b.13%252C_p.443_-_Council_in_Trullo.gif&w=640&q=50)
Mtaguso wa tano-sita
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mtaguso wa tano-sita (au Mtaguso wa Trulo, yaani wa kuba, kwa kuwa ulikutanika ikulu) ni mtaguso uliofanyika Konstantinopoli chini ya kaisari Justiniani II mwaka 692. Uliitwa wa tano-sita kwa sababu ulitarajiwa kukamilisha mitaguso ya kiekumene wa tano na wa sita kwa kutoa sheria ambazo hiyo mitaguso haikuzitunga.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/9/9d/Facial_Chronicle_-_b.13%2C_p.443_-_Council_in_Trullo.gif/640px-Facial_Chronicle_-_b.13%2C_p.443_-_Council_in_Trullo.gif)
Walishiriki maaskofu 215, karibu wote kutoka Dola la Roma Mashariki.
Papa Sergio I alikataa kabisa[1][2] kuthibitisha kanuni hizo [3] zikilenga kufanya desturi za Konstantinopoli zifuatwe na Wakatoliki wote[4][5]. Kwa sababu hiyo kaisari aliagiza akamatwe na kuletwa Konstantinopoli, lakini watu walizuia utekelezaji wa amri hiyo[6][7].