![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/sw/thumb/1/1a/Straight-outta-compton-nwa-movie.jpg/640px-Straight-outta-compton-nwa-movie.jpg&w=640&q=50)
N.W.A
From Wikipedia, the free encyclopedia
N.W.A (kifupisho cha Niggaz Wit Attitudes)[1][2][3] lilikuwa kundi la muziki wa hip hop kutoka mjini Compton, California, nchini Marekani. Kundi hili hutazamiwa kama miongoni mwa makundi yaliyochochea mtindo wa gangsta rap,[4] wakati mwingine hutazamiwa tena kama kundi muhimu sana katika historia nzima ya muziki wa hip hop.[5] Lilianza kazi zake tangu mwaka wa 1986 hadi 1991, kundi lilizua minong'ono ya hapa na pale hasa kwa hali halisi ya mashairi yao makali, na hatimaye kufungiwa nyimbo zao zisipigwe katika vituo kadha wa kadha huko nchini Marekani. Licha ya hilo kutokea, kundi liliuza nakala zaidi ya milioni 10 ya CD kwa Marekani pekee. Kutokana na ukatili wa polisi na ukosefu wa usawa wa rangi katika maeneo wanayotokea wanachama wake, kundi hili lilitengeneza muziki wa kisiasa. [6]Wanachama wa kundi hili walionyesha wazi kuchukia mfumo wa polisi, mfumo ambao umezua mijadala mingi kwa miaka mingi.
N.W.A | |
---|---|
![]() | |
Maelezo ya awali | |
Asili yake | South Central Los Angeles, Compton, California, Marekani |
Aina ya muziki | Hip hop |
Miaka ya kazi | 1986–1991 1999–2000 (Muungano wa Muda) |
Studio | Ruthless, Priority, EMI |
Ame/Wameshirikiana na | Above the Law, Bobby Jimmy and the Critters, C.I.A., Fila Fresh Crew, J. J. Fad, Snoop Dogg, The D.O.C., World Class Wreckin' Cru |
Wanachama wa sasa | |
Eazy-E Dr. Dre Ice Cube DJ Yella MC Ren Arabian Prince |
Kundi linaunganishwa na mtu kama Arabian Prince, DJ Yella, Dr. Dre, Eazy-E, Ice Cube, na MC Ren. Walitoa albamu ya mkusanyiko ya kwanza kama kundi mnamo mwaka 1987, iliitwa N.W.A. and the Posse na ilishika nafasi ya 39 kwenye chati ya Albamu bora za R&B/Hip-Hop inayochapishwa na jarida la Billboard. Arabian Prince alijitoa muda mfupi baada ya kutolewa kwa studio albamu ya kwanza ya N.W.A, Straight Outta Compton, mwaka wa 1988, huku Ice Cube naye akifuata nyayo mnamo Desemba 1989 kwa sababu za mgogoro wa kimaslahi. Wanachama mbalimbali wa kundi hili baadaye wakaja kuuza nakala zilizofikia kiwango cha platinamu katika miaka ya 1990. Albamu ya kwanza ya kundi imenakiliwa kama mwanzo wa zama mpya za Gangsta rap kwani utayarishaji wake na maoni ya kijamii katika mashairi yao yalikuwa mapinduzi makubwa ndani ya mtindo huu.[7] Studio albamu ya pili ya N.W.A, Niggaz4Life, ilifika namba moja kwenye chati za mauzo za Billboard 200.[8]
Rolling Stone iliiorodhesha N.W.A katika nafasi ya 83 kwenye orodha yake ya "Wasanii Wakubwa 100 wa wakati wote". [9]Mnamo mwaka wa 2016, kundi hili liliingizwa kwenye Jumba la Umaarufu la Rock na Roll, baada ya kupendezwa mara tatu hapo awali.