Oswald wa Northumbria
From Wikipedia, the free encyclopedia
Oswald wa Northumbria (Deira, Northumbria, 604 hivi ā Maserfield, 5 Agosti 641/642[1]) alikuwa mfalme wa Northumbria kuanzia mwaka 634 hadi kifo chake vitani. Aliunganisha tena nchi na kueneza Ukristo ndani yake[2].
Ni kwamba mwaka 616 alilazimishwa kwenda uhamishoni katika kisiwa cha Iona ambako akabadilika kuwa Mkristo na kubatizwa.
Mwaka 634 Oswald alirudishiwa ufalme wa Northumbria akaamua kuwaingiza katika Ukristo wananchi wake ambao wengi wao walikuwa Wapagani. Ili kutekeleza lengo hilo aliwaomba watawa wa Iona wamtumie wamisionari, naye Aidani wa Lindisfarne akafika mwaka 635.
Aidan alichagua kisiwa cha Lindisfarne kiwe makao makuu ya dayosisi yake kwa vile kilikuwa karibu na ngome ya kifalme kule Bamburgh.
Mwanzoni alikuwa mfalme Oswald mwenyewe aliyewatafsiria Aidan na watawa wake kwa vile walikuwa hawajajifunza lugha ya kale ya Kiingereza.
Jamadari hodari, ingawa alipenda zaidi amani, aliuawa na Wapagani waliomchukia Yesu Kristo.
Habari zake ziliandikwa hasa na Beda Mheshimiwa Archived 22 Novemba 2001 at the Wayback Machine..
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana kama mtakatifu mfiadini[3][4].