Papa Urban V
From Wikipedia, the free encyclopedia
Papa Urban V, O.S.B. (takriban 1310 – 19 Desemba 1370) alikuwa Papa kuanzia tarehe 28 Septemba/6 Novemba 1362 hadi kifo chake[1]. Alitokea Grizac, Ufaransa[2].
Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Guillaume Grimoard.
Alimfuata Papa Innocent VI akafuatwa na Papa Gregori XI. Alikuwa wa sita kati ya Mapapa walioishi Avignon, na alirudi Roma kwa muda hadi aliposhindwa na mazingira.
Alisifiwa kwa elimu na utakatifu wake.
Alitangazwa mwenye heri na Papa Pius IX tarehe 10 Machi 1870.