Kanghagha au zogoyogo ni ndege wa familia Leiotrichidae. Wanafanana na mikesha wa familia Turdidae. Wanatokea misitu na maeneo mengine yenye miti katika Afrika na Asia. Spishi za Afrika zina rangi za kahawa, nyeusi, kijivu na nyeupe, lakini spishi nyingi za Asia zina rangi kali pia kama nyekundu na njano. Takriban spishi zote huenda kwa makundi wakiwasiliana kwa sauti. Mara kwa mara hupiga kelele sana, kwa sababu yake huitwa mpayupayu pia (“babbler” au “chatterer” kwa Kiingereza). Hula wadudu hasa lakini beri pia; spishi kubwa hula mijusi na panya wadogo na spishi kadhaa hula beri tu. Hulijenga tago lao kwa vitawi na kulificha katika vichaka vizitu. Jike huyataga mayai 2-5. Spishi kadhaa hujenga tago kwa kundi; jike mmoja tu hutaga mayai na ndege wengine husaidia kuwalinda makinda na kuwaletea chakula.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Kanghagha |
Zogoyogo wa Sharpe |
Uainishaji wa kisayansi |
|
Ngazi za chini |
Jenasi 13:
- Actinodura Gould, 1836
- Argya Lesson, 1831
- Cutia Hodgson, 1837
- Garrulax Lesson, 1831
- Heterophasia Blyth, 1842
- Ianthocincla Gould, 1835
- Laniellus Swainson, 1832
- Leiothrix Swainson, 1832
- Liocichla Swinhoe, 1877
- Minla Hodgson, 1837
- Pterorhinus Swinhoe, 1868
- Trochalopteron Blyth, 1843
- Turdoides Cretzschmar, 1827
|
Funga
- Argya aylmeri, Kanghagha Mabaka (Scaly Chatterer)
- Argya fulva, Kanghagha Kahawiachekundu (Fulvous Babbler)
- Argya rubiginosa, Kanghagha tumbo-kahawianyekundu (Rufous Chatterer)
- Turdoides atripennis, Kanghagha Kichwa-kijivu (Capuchin Babbler)
- Turdoides bicolor, Kanghagha Rangi-mbili (Southern Pied Babbler)
- Turdoides chapini, Kanghagha-milima wa Chapin (Chapin's Babbler)
- Turdoides gilberti, Kanghagha-milima Koo-jeupe (White-throated Mountain Babbler)
- Turdoides gymnogenys, Kanghagha Shavu-wazi (Bare-cheeked Babbler)
- Turdoides hartlaubii, Kanghagha wa Angola (Hartlaub's au Angola Babbler)
- Turdoides hindei, Zogoyogo wa Hinde (Hinde's Babbler)
- Turdoides hypoleuca, Kanghagha Tumbo-jeupe (Northern Pied Babbler)
- Turdoides jardineii, Zogoyogo (Arrow-marked Babbler)
- Turdoides leucocephala, Kanghagha Kichwa-cheupe (White-headed au Cretschmar's Babbler)
- Turdoides leucopygia, Kanghagha Kiuno-cheupe (White-rumped Babbler)
- Turdoides melanops, Zogoyogo Uso-mweusi (Black-faced Babbler)
- Turdoides plebejus, Kanghagha Kahawia (Brown Babbler)
- Turdoides reinwardtii, Kanghagha Kichwa-cheusi (Blackcap Babbler)
- Turdoides rufocinctus, Kanghagha-milima Mkufu-mwekundu (Red-collared Babbler)
- Turdoides sharpei, Zogoyogo wa Sharpe au Damisi (Black-lored au Sharpe's Pied Babbler)
- Turdoides squamulata, Kanghagha Madoadoa (Scaly Babbler)
- Turdoides tenebrosa, Kanghagha Mweusi (Dusky Babbler)
Grey-cheeked fulvetta
Mountain fulvetta
Javan fulvetta
Black-throated laughingthrush
Yellow-throated laughingthrush
Greater necklaced laughingthrush
Masked laughingthrush
Chinese hwamei
Spectacled laughingthrush
Black-chinned laughingthrush
Streaked laughingthrush
Red-winged laughingthrush
White-whiskered laughingthrush
Variegated laughingthrush
Yellow-billed babbler
Common babbler
Striated babbler
White-throated babbler
Large grey babbler
Orange-billed babbler
Arabian babbler
Jungle babbler
Rufous babbler