![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/9/99/Penicillin_core.svg/langsw-640px-Penicillin_core.svg.png&w=640&q=50)
Penisilini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Penisilini (wakati mwingine hujulikana kwa ufupi kama PSN) ni kundi la dawa za antibiotiki zinazotokana na kuvu Penicillium chrysogenum. Penisilini zote ni antibiotiki za Beta-laktami na zinatumika kwa kutibu maambukizi yanayosababishwa na bakteria zinazoweza kuathiriwa, kwa kawaida bakteria za aina Gram-chanya.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/9/99/Penicillin_core.svg/320px-Penicillin_core.svg.png)
Antibiotiki za penisilini zina umuhimu wa kihistoria kwa sababu ni dawa za kwanza zilizokuwa na manufaa kwa kukinga magonjwa mengi za hapo mbeleni zilizokuwa na uzito, kwa mfano magonjwa kama kaswende na maambukizi ya Staphylococcus.
Penisilini bado zinatumika sana leo, ijapokuwa aina nyingi za bakteria sasa hazisikii dawa hiyo.