Ramadan (mwezi)
mwezi mtukufu wa mfungo kwa Waislamu, unaoadhimishwa katika mwezi wa tisa wa kalenda ya Kiislamu / From Wikipedia, the free encyclopedia
Ramadan au ramadhani, (kwa Kiarabu: رمضان) ni mwezi wa tisa katika Kalenda ya Kiislamu na mwezi wa kufunga katika Uislamu kuadhimisha ufunuo wa kwanza wa Qur'an kutona na mafundisho ya Mtume Muhammad. Mwezi huo huwa na siku 29 au 30 kutegemeana na kuonekana kwa mwezi.
Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya |
Imani na ibada zake |
Umoja wa Mungu |
Waislamu muhimu |
Abu Bakr • Ali |
Maandiko na Sheria |
Qur'an • Sunnah • Hadithi |
Historia ya Uislamu |
Historia |
Tamaduni za Kiislamu |
Shule • Madrasa |
Tazama pia |
Uislamu na dini nyingine |
.
Kufunga ni moja ya Nguzo tano za Uislamu. Mwislamu mzima, mwenye afya nzuri, anatakiwa kushiriki katika swaumu ambayo ni ibada ya kufunga chakula na kinywaji mchana kutwa, pamoja na kujizuia kufanya mapenzi toka alfajiri hadi magharibi.
Matendo hayo ya toba yanaendana na kuswali sana na kusoma Quran kwa wingi.
Kwa wagonjwa, wanaosafiri, wazee, wajawazito, wanaonyonyesha na wanawake wenye hedhi sio lazima kufunga.
Mwisho wa Ramadhani ni sikukuu ya Idul Fitri (عيد الفطر - ʿīdu ʾl-fiṭr) ambayo ni sherehe ya furaha na kupongezana. Waislamu hutoa zakat (zakatul-fitri زكاة الفطر) na kuswali, baadaye hukutana kwenye karamu.
Neno Ramadhani linatokana na mizizi ya Kiarabu ramiḍa au ar-ramaḍ, ambayo inamaanisha joto kali au ukavu.[1]