Siku ya kimataifa ya vijana
From Wikipedia, the free encyclopedia
Siku ya kimataifa ya vijana (kwa Kiingereza: World Youth Day; kifupi: WYD) ni tukio linaloandaliwa na Kanisa Katoliki kwa ajili ya rika hilo. Kila mwaka siku ya vijana inaadhimishwa ama katika majimbo tu kwenye Jumapili ya matawi, ama kimataifa katika mji fulani.
Maelezo zaidi Imani, Muundo ...
Funga
Mpango huo ulianzishwa na Papa Yohane Paulo II mwaka 1985 kwa kufuata mang'amuzi yake nchini Polandi [1] ukaendelezwa na waandamizi wake, Papa Benedikto XVI [2] na Papa Fransisko.
Misa ya kumalizia adhimisho hilo mjini Manila, Ufilipino, mwaka 1995 ilihudhuriwa na watu milioni 5.