Abacavir

From Wikipedia, the free encyclopedia

Abacavir
Remove ads

Abacavir, inayouzwa chini ya jina la chapa Ziagen, ni dawa inayotumika kuzuia na kutibu HIV/UKIMWI.[1][2] Sawa na vizuizi vingine vya nucleoside analog reverse-transcriptase (NRTIs), abacavir hutumiwa pamoja na dawa zingine za HIV, na haipendekezwi yenyewe tu.[3] Inachukuliwa kwa mdomo kama tembe au kiowevu na inaweza kutumika kwa watoto zaidi ya umri wa miezi mitatu.[1][4]

Ukweli wa haraka Jina la (IUPAC), Data ya kikliniki ...

Abacavir kwa ujumla inavumiliwa vizuri. [4] Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kutapika, shida ya kulala, homa na kuhisi uchovu.[1] Madhara yake makubwa zaidi ni pamoja na hisia kali(hypersensitivity), uharibifu wa ini na kuongezeka kwa asidi ya lactic mwilini (lactic acidosis).[1] Uchunguzi wa maumbile unaweza kuonyesha ikiwa mtu yuko katika hatari kubwa ya kupatwa na hisia kali (hypersensitivity).[1] Dalili za hisia kali ni pamoja na upele, kutapika na upungufu wa kupumua.[4] Abacavir iko katika kundi la dawa za NRTI, ambazo hufanya kazi kwa kuzuia nakala rudufu ya nyuma (reverse transcriptase), kimeng'enya kinachohitajika kwa ajili ya uzalishaji wa virusi vya HIV.[5] Ndani ya kundi la NRTI, abacavir ni nukleosidi ya karbosikliki (nucleoside ya carbocyclic).[1]

Abacavir ilipewa hati miliki mwaka wa 1988, na kuidhinishwa kutumika nchini Marekani mwaka wa 1998.[6][7] Iko kwenye Orodha ya Dawa Muhimu ya Shirika la Afya Ulimwenguni.[8] Inapatikana kama dawa ya kawaida.[1] Gharama ya jumla katika nchi zinazoendelea kufikia mwaka wa 2014 ilikuwa kati ya dola za Marekani 0.36 na 0.83 kwa siku.[9] Kufikia mwaka wa 2016, gharama ya jumla kwa mwezi wa kawaida wa dawa nchini Marekani ni dola 70.50.[10] Kwa kawaida, abacavir huuzwa pamoja na dawa zingine za HIV, kama vile abacavir/lamivudine/zidovudine, abacavir/dolutegravir/lamivudine na abacavir/lamivudine.[4][5] Mchanganyiko wa abacavir/lamivudine pia ni dawa muhimu.[8]

Remove ads

Marejeleo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads