Akademia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Akademia (kutoka neno la Kigiriki Ἀκαδήμεια, ambalo baadaye likawa Ἀκαδημία akademia) ni shule au chuo kinachotoa elimu au taaluma maalumu, k.v. lugha, muziki, michezo au sanaa.

Jina linarejelea taasisi iliyoundwa na Plato kwenye mwaka 385 KK ilikuwa chuo chake cha falsafa mjini Athens iliyokuwepo ndani ya hekalu ya Athena, mungu wa hekima na elimu.
Pia inaweza kuwa kundi la wasomi wenye ujuzi mkubwa katika taaluma fulani, k.v. siasa, uchumi au masuala ya jamii.
Tena inaweza kuwa taasisi rasmi inayohamasisha maendeleo ya fasihi, sayansi n.k.
Nchi nyingi huwa na "Akademia ya Sayansi" ambayo ni shirika za wataalamu au pia taasisi za wataalamu. Zinalenga kujenga na kuimarisha ushirikiano wa wataalamu wa fani mbalimbali, mbali na kazi yao kwenye vyuo vikuu[1]. Akademia ya Sayansi hailengi kufundisha, inalenga kuunganisha wataalamu na tafiti zao.
Remove ads
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads