Algorithimu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Algorithimu
Remove ads

Algorithimu (pia: algoriti kutoka Kiingereza: Algorithm) ni utaratibu wa hatua-kwa-hatua wa kutatua tatizo haswa tatizo la kihesabu [1], yaani ni kanuni au maelekezo ya hesabu ambayo kama yakifuatwa na kompyuta yanaweza yakapata jibu la tatizo [2], hivyo ni njia ya kutatua kwa hatua chache magumu katika hisabati. Njia hiyo inaweza kufanya hesabu na usindikaji wa data.

Thumb
Uhaishaji wa algoriti ya QuickSort ikipanga safu zilizowekwa kiholela.

Algoriti inaweza kutumika kwenye kazi rahisi kama kupanga orodha ya namba au kwenye majukumu tata kama kutoa mapendekezo ya mahudhui kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii. Algoriti hufanya kazi kwa kufata maelekezo au kanuni za kutekeleza jukumu au kutatua tatizo, zinawezwa andikwa kwa kutumia lugha ya asili, lugha ya programu, msimbo bandia, na chati mtiririiko.

Lugha ya asili huwa haitumiki sana kuandika algoriti kwasababu ya utata wake, lugha ya programu hutumika zaidi kuandika algoriti ambayo huchakatwa na kompyuta [3].

Jina linatokana na mwanahisabati wa Uajemi al-Khwarizmi aliyetoa maelekezo ya kwanza ya namna hiyo katika karne ya 9 BK.

Remove ads

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads