Tairi (nyota)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kuhusu kifaa kinachotumiwa kwenye gari angalia hapa tairi


Tairi (kwa Kiingereza na Kilatini Altair al-tair, pia α Alpha Aquilae, kifupi Alpha Aqu, α Aqu) ni nyota angavu zaidi katika kundinyota la Ukabu (Aquila). Ni pia nyota angavu ya 12 kabisa kwenye anga la usiku. Mwangaza unaoonekana ni mag 0.77. Tairi ni sehemu ya Pembetatu ya Kiangazi kwenye angakaskazi.
Remove ads
Jina
Tairi ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [1]. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema النسر الطائر an-nasr al-tair ambalo linamaanisha “ndege aina ya tai anayepuruka” wakitaja ama kundinyota lote au hasa nyota tatu za a = Tairi, b na g. Hii ilikuwa namna yao ya kutafsiri jina la Kigiriki Ἀετός a-e-tos yaani tai walilolikuta kwa Ptolemaio katika kitabu chake cha Almagesti. Wagiriki waliwahi kupokea kundinyota hili kutoka Wababeli ambao waliona hapa pia ndege mkubwa kwenye anga.
Wataalamu wa Ulaya walipokea jina la Kiarabu kwa ajili ya nyota angavu zaidi na hapa walitumia sehemu ya jina “al-tair” pekee. Kwa Kiarabu neno hili linamaanisha “mwenye kurupuka” na kwa kundinyota walitumia tafsiri ya jina la Kigiriki lenyewe kwa Kilatini “Aquila”.
Remove ads
Tabia
Tairi - Altair ni nyota ya jamii A kwenye safu kuu. Mwangaza unaoonekana ni mag 0.77 na mwangaza halisi ni 2.22. [2]. Umbali wake na Dunia ni miaka nuru 16.7 [3].
Masi yake ni M☉ 1.79 na nusukipenyo chake R☉ 1.58 (vizio vya kulinganisha na Jua letu) [4].
Tairi ni nyota inayozunguka haraka kwenye mhimili wake. Mzunguko mmoja una muda wa saa 9 pekee (kwa kulinganisha: Jua letu linazunguka kwenye mhimili wake katika muda wa siku 25). Kasi kubwa ya mzunguko inabadilisha umbo la Tairi kufanana na mpira unaokazwa, si tufe. Maana kipenyo kwenye ikweta yake iko 20% kuliko kipenyo kwenye ncha zake. [5]
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads