Amber Midthunder

Mwigizaji wa Marekani From Wikipedia, the free encyclopedia

Amber Midthunder
Remove ads

Amber Midthunder (amezaliwa Aprili 26, 1997)[1] ni mwigizaji wa Marekani. Anajulikana katika kuigiza kwenye tamthilia kama FX Legion, Roswell na New Mexico, pia alionekana katika filamu ya Longmire, Banshee, na Reservation Dogs[2][3][4]. Aliigiza kama Naru katika filamu ya Prey.[5]

Ukweli wa haraka
Thumb

Maisha ya zamani

Mama yake Midthunder aitwaye Angelique, ana asili ya Thailand na China ni mwongozaji wa filamu[6], na baba yake David ni mwigizaji mwenye asili ya Marekani. Angelique na David walikutana wakiwa wanafanya kazi katika filamu ya Kijapani iitwayo East Meets West ya mwaka 1995.[7]

Midthunder ni raia wa Fort Peck Assiniboine na kabila la Sioux[8][9][10]. Alizaliwa katika taifa la Navajo la Shiprock, New Mexico, aliamua kurudi baada ya kutumia mda mwingi wa utoto wake huko Santa Fe ambako alihudhuria katika chuo cha Teknolojia ambapo mama yake alifanya kazi katika kampuni ya uigizaji.[11]

Remove ads

Kazi

Midthunder akiwa mtoto alikua na shauku ya kuigiza, ambapo alikariri mistari kutoka kwenye maonyesho na filamu alizozipenda, lakini hakupenda utendaji wake wa kazi kwa mara ya kwanza na hivyo aliamua kuchukua mda kabla ya kushiriki kazi zingine[12]. Alianza kupata umaarufu katika filamu ya Sunshine Cleaning ya 2008. Midthunder aliendelea kufanya kazi katika mashirika ya uandaaji wa filamu huko New Mexico kabla ya kwenda Los Angeles akiwa na umri wa miaka 17 ili kutafuta fursa zaidi za uigizaji. Aliigiza kama Naru katika filamu ya Prey ambayo ni mfululizo wa tano katika filamu za Predator.

Remove ads

Tuzo

Mnamo mwaka 2021, Midthunder alipokea tuzo ya Utendaji Bora katika Tuzo za Saturn[13] na pia alichaguliwa kuwania tuzo za Critics Choice Awards katika kipengele cha Mwigizaji bora wa kike katika filamu za Televisheni.[14]

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads