Buibui-mjeledi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Buibui-mjeledi (kutoka Kiing. whip spider) ni arithropodi wa oda Amblypygi katika ngeli Arachnida wafananao na buibui wa kawaida. Kama hawa wana miguu minane lakini hawawezi kusokota nyuzi za hariri. Mwili wao una sehemu mbili kama buibui: kefalotoraksi (cephalothorax: kichwa na kidari) na fumbatio zilizoungwa kwa pediseli (pedicel) nyembamba kwa umbo wa mrija. Mgongo wa kefalotoraksi ni ngumu na kwa hivyo huitwa gamba (carapace). Kinyume na buibui kelisera (chelicerae) za buibui-mjeledi ni fupi na pedipalpi ni ndefu zenye gando kama kaa. Pedipalpi hutumika kwa kukamata mawindo na kelisera kwa kuyakatakata. Miguu sita tu hutumika kwa kutembea. Jozi ya kwanza imekuwa miembamba na mirefu sana mpaka zaidi ya mara nne urefu wa mwili (inafanana na mijeledi, asili ya jina lao) na hutumika kama vipapasio. Buibui-mjeledi hula arithropodi wengine.
Remove ads
Spishi za Afrika
- Charinus africanus
- Charinus abbatei
- Charinus fagei
- Charinus kakum
- Charinus madagascariensis
- Charinus milloti
- Charinus seychellarum
- Charinus socotranus
- Damon annulatipes
- Damon brachialis
- Damon diadema
- Damon gracilis
- Damon johnstonii
- Damon longispinatus
- Damon medius
- Damon sylviae
- Damon tibialis
- Damon uncinatus
- Damon variegatus
- Euphrynichus amanica
- Euphrynichus bacillifer
- Musicodamon atlanteus
- Phrynichodamon scullyi
- Phrynichus brevispinatus
- Phrynichus deflersi
- Phrynichus exophthalmus
- Phrynichus longespina
- Phrynichus madagascariensis
- Phrynichus scaber
- Phrynichus spinitarsus
- Xerophrynus machadoi
Picha
- Charinus vulgaris (Charinidae)
- Charinus kakum (Charinidae)
- Damon diadema (Phrynichidae)
- Damon medius (Phrynichidae)
- Damon variegatus (Phrynichidae)
- Phrynichus phipsoni (Phrynichidae)
- Paraphrynus mexocanus (Phrynidae)
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads