Ampicillin
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ampicillin ni antibiotiki inayotumika kuzuia na kutibu idadi ya maambukizo ya bakteria, kama vile maambukizo ya njia ya upumuaji, maambukizi ya mfumo wa mkojo, uti wa mgongo, maambukizi ya njia ya chakula yanaosababishwa na bakteria aina ya Salmonella (salmonellosis), na maambukizi ya utando wa ndani wa moyo (endocarditis).[2] Inaweza pia kutumika kuzuia maambukizi ya bakteria wa streptococcus (streptococcal) ya kikundi B kwa watoto wachanga.[2] Inatumiwa kwa mdomo, kwa sindano kwenye misuli, au kwa njia ya mishipa.[2] Kama viua vijasumu vyote, haina ufanisi kwa matibabu ya maambukizo ya virusi.
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na upele, kichefuchefu na kuhara.[2] Haipaswi kutumiwa kwa watu ambao wana mzio wa penicillin.[2] Madhara yake makubwa yanaweza kujumuisha Clostridium difficile colitis au anaphylaxis.[2] Ingawa inaweza kutumika kwa wale walio na matatizo ya figo, dozi inaweza kuhitajika kupunguzwa.[2] Matumizi yake wakati wa ujauzito na unyonyeshaji yanaonekana kuwa salama kwa ujumla.[2][3]
Ampicillin iligunduliwa mwaka wa 1958 na ilianza kufanyiwa biashara mwaka wa 1961.[4][5] Iko kwenye Orodha ya Dawa Muhimu ya Shirika la Afya Ulimwenguni.[6] Gharama yake ya jumla katika nchi zinazoendelea ilikuwa kati ya Dola za Marekani 0.13 na 1.20 kwa chupa ya myeyusho wa mishipani kufikia mwaka wa 2014.[7] Nchini Marekani, inapatikana kama dawa ya kawaida na gharama ya matibabu ya siku 10 ni takriban $13.[2]
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads