Unyonyeshaji

From Wikipedia, the free encyclopedia

Unyonyeshaji
Remove ads
Remove ads

Kunyonyesha ni ulishaji wa watoto wachanga na wadogo kwa maziwa kutoka kwenye titi la mwanamke.[1]

Thumb
Mtoto akinyonya
Muhtasari wa video ya makala na chapisho.

Wataalamu wa afya wanapendekeza kunyonyesha kuanzia saa ya kwanza ya maisha ya mtoto na kuendelea mara nyingi na kwa kadiri mtoto anavyotaka.[2][3] Katika wiki chache za kwanza za maisha watoto wanaweza kunyonya takriban kila masaa mawili hadi matatu, na muda wa unyonyaji kwa kawaida ni dakika kumi hadi kumi na tano kwa kila titi.[4] Watoto wakubwa hula kidogo mara nyingi.[5]

Akina mama wanaweza kukamua maziwa ili yaweze kutumika baadaye wakati ambapo unyonyeshaji hauwezekani.[1] Kunyonyesha kuna faida kadhaa kwa mama na mtoto, ambayo fomula ya watoto wachanga hukosa.[3][6]

Vifo vya takriban watoto 820,000 walio chini ya umri wa miaka mitano vinaweza kuzuilika duniani kila mwaka kutokana na kuongezeka kwa unyonyeshaji. [7] Kunyonyesha kunapunguza hatari ya maambukizi ya mfumo wa upumuaji na kuhara kwa mtoto, katika nchi zinazoendelea na zilizoendelea. [2] [3] Faida nyingine ni pamoja na hatari ndogo za pumu, mizio ya chakula, na kisukari aina ya 1 . [3] Kunyonyesha kunaweza pia kuboresha ukuaji wa utambuzi na kupunguza hatari ya unene wa kupindukia katika utu uzima. [2] Akina mama wanaweza kuhisi shinikizo la kunyonyesha, lakini katika dunia iliyoendelea watoto kwa ujumla hukua kawaida wanapolishwa kwa chupa na mchanganyiko wa maziwa ya kutengeneza. [8]

Manufaa kwa mama ni pamoja na kupoteza damu kidogo baada ya kujifungua, usinyaaji bora wa uterasi, na kupungua kwa mfadhaiko baada ya kujifungua. [3] Kunyonyesha huchelewesha kurudi kwa hedhi na uwezo wa kushika mimba, jambo linalojulikana kama amenorrhea ya unyonyeshaji. [3] Manufaa ya muda mrefu kwa mama ni pamoja na kupungua kwa hatari ya saratani ya matiti, ugonjwa wa moyo, na baridi yabisi. [3] [7] Kunyonyesha maziwa ya mama pia ni nafuu kuliko fomula ya watoto wachanga. [9] [10]

Mashirika ya afya, yakiwa ni pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO), yanapendekeza kunyonyesha pekee kwa miezi sita. [2] [3] [11] Hii ina maana kwamba hakuna vyakula au vinywaji vingine, isipokuwa ikiwezekana vitamini D, ambavyo vitolewe kwa kawaida. [12] Baada ya kuanzishiwa vyakula katika umri wa miezi sita, mapendekezo mengine ni pamoja na kuendelea kunyonyesha hadi umri wa mwaka mmoja hadi miwili au zaidi. [2] [3] Ulimwenguni, takriban 38% ya watoto wachanga hunyonyeshwa tu katika miezi sita ya kwanza ya maisha. [2] Nchini Marekani mwaka wa 2015, 83% ya wanawake walianza kunyonyesha, lakini katika miezi 6 ni 58% tu waliokuwa bado wananyonyesha huku 25% wakinyonyesha peke yake. [13]

Hali za tiba ambazo haziruhusu kunyonyesha ni chache. [3] Akina mama wanaotumia dawa fulani za kujivinjari na matibabu hawapaswi kunyonyesha. [14] [15] Kuvuta tumbaku na kutumia kiasi kidogo cha pombe na/au kahawa si sababu za kuepuka kunyonyesha. [16] [17] [18]

Remove ads

Marejeo

Loading content...
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads