Anafora ni jina la matini ya sehemu muhimu zaidi ya Liturujia ya Kimungu (au Misa), ambapo vipaji vya mkate na divai pamoja na maji kidogo vinageuzwa na Roho Mtakatifu kuwa mwili na damu ya Yesu Kristo kadiri ya imani ya Wakristo wengi, hasa Wakatoliki na Waorthodoksi.


Jina hilo linatumiwa hasa katika Ukristo wa Mashariki, wakati madhehebu mengine yanasema zaidi sala ya ekaristi.
"Anafora" ni neno la Kigiriki ἀναφορά, anafora, maana yake "kuchukua nyuma" au "kuchukua juu", na hivyo pia "toleo"[1] hasa kwa maana ya sadaka inayotolewa kwa Mungu).
Muundo wa anafora ni tofautitofauti, hasa kufuatana na mapokeo ambayo yalifikia hatua muhimu katika karne ya 4 na kufuatwa hata leo[2][3], ingawa Uprotestanti uliachana nayo kwa muda mrefu.
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.