Mnanasi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mnanasi
Remove ads

Mnanasi (Ananas comosus) ni mmea katika familia Bromeliaceae ya oda Poales.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...

Mnanasi unakuzwa hasa kwa sababu ya matunda yake, yanayoitwa mananasi, na juisi inayotokana na matunda haya.

Asili yake ni Amerika ya Kusini ingawa kwa sasa unakuzwa sehemu nyingi za dunia.

Remove ads

Visumbufu vya mnanasi

Vijidudu vinavyomelea mnanasi huchangia kuleta hasara kubwa kote duniani katika uzalishaji wa mananasi[1]. Spishi zaidi ya mia moja za nematodi zimeripotiwa kuingia mizizi ya mnanasi[1] na kutatiza matumizi ya madini na maji kwa mmea na kusababisha mimea kudumaa. Aina za vijidudu hivi ambavyo huadhiri mavuno ya mananasi sana ni spishi za nematodi kama vile Meloidogyne javanica, M. incognita, Rotylenchulus reniformis na Pratylenchus brachyurus[2][1].

Helicotylenchus dihystera na Criconemella ornata (kwa Kiing. Ring nematode) pia hupatikana sana kwa mashamba ya mananasi ingawa huwa hawasababishi uharibifu wowote uonekanao[3] [4].

Huko Hawaii, upungufu wa kiasi kikubwa wa uzalishaji wa mananasi umeripotiwa kutokana na uharibifu au maambukizo ya nematodi. Katika mashamba ya mananasi ya Queensland, huko Australia, M. javanica ameripotiwa kuwa spishi aliye na uharibifu zaidi kuliko aina zote za vijidudu vinavyomelea mananasi[4].

Remove ads

Picha

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads