Apoloni na Filemoni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Apoloni na Filemoni (walifariki karibu na Antinoe, 307 hivi) walikuwa Wakristo wa Misri waliofia imani yao wakati wa dhuluma ya kaisari Diokletian.

Apoloni alikuwa mmonaki shemasi, kumbe Filemoni alikuwa mwanamuziki aliyemtukana na kumdhihaki. Kwa kuona alivyojibiwa kila mara kwa upole na wema aliongokea Ukristo na kujitambulisha kwa hakimu. Hatimaye waliuawa pamoja [1].
Wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads