Ibn Sina

From Wikipedia, the free encyclopedia

Ibn Sina
Remove ads

Ibn Sina (pia: Avicenna; jina kamili: Abū ʿAlī al-Ḥusayn ibn ʿAbd Allāh ibn Sīnā; kwa Kiarabu ابو علی الحسین ابن عبدالله ابن سینا) ni kati ya wataalamu na wanafalsafa mashuhuri kabisa katika historia ya Uislamu.

Thumb

Alizaliwa mnamo mwaka 980 karibu na mji wa Bukhara [1][2] katika Khorasan (leo nchini Uzbekistan) akafa mwaka 1037 mjini Hamadan [3][4]) katika Uajemi.

Alishughulika sayansi nyingi; alikuwa tabibu na pia mtaalamu wa fizikia, sheria, hisabati, astronomia na kemia.

Kwa jumla alitoa maandiko 450 kuhusu mada mbalimbali na 240 kati ya haya zimepatikana hadi leo. Vitabu vilitafsiriwa kwa lugha mbalimbali hata kwa Kilatini na kwa njia hiyo Ibn Sina alikuwa pia mwalimu wa Ulaya katika tiba na falsafa.

Remove ads

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads