Awasa

From Wikipedia, the free encyclopedia

Awasa
Remove ads

Awasa (pia Awassa au Hawassa, Kige'ez አዋሳ) ni mji mkuu wa Jimbo la Mataifa ya Kusini katika kusini ya Ethiopia. Iko kando la Ziwa Awasa katika Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki takriban kilomita 280 kusini ya Addis Abeba.

Thumb
Soko la samaki kando la ziwa mjini Awasa
Thumb
Mahali pa Awasa nchini Ethiopia
Thumb
Ramani ya mji wa Awasa

Mwaka 2005 Awasa ilikuwa na wakazi 125,315.[1]

Kati ya wakazi wake 69,169 wa mwaka 1994 asilimia 31,42 % walikuwa Waamhara, 24,91 % Wawelaytta, 11,55 % Waoromo, 10,2 % Wasidama, 4,85 % Wakambaata, 4,6 % Watigray, 3,23 % Soddo-Gurage, 2,15 % Wasilt'e, 2,13 % Sebat-Bet-Gurage und 1,56 % Wahadiyya.

63,42 % walisema Kiamhara kama lugha ya kwanza. [2]

Kiasili eneo la Awasa ilikuwa na misitu minene na hadi leo kuna miti mikubwa upande wa kaskazini na magharibi wa mji. Kuna maji mengi kwa hiyo watu wengi kutoka nyanda za juu walihamia hapa.

Awasa ilikuwa mji mkuu wa jimbo la awali la Sidamo. [3]

Barabara kuu kati na Addis Abeba na Nairobi inapita Awasa.

Uvuvi katika ziwa ni sehemu muhimu ya uchumi kwa wenyeji.

Kuna vyuo viwili ambavyo ni Awasa Adventist College na Chuo Kikuu cha Awasa.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads