Nairobi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Nairobi
Remove ads

Nairobi ni mji mkuu na jiji kubwa zaidi la Kenya, lililoko katika sehemu ya kusini-kati ya nchi. Jina lake limetokana na usemi wa Kimaasai "Enkare Nairobi," maana yake "maji baridi," likirejelea Mto Nairobi unaopita katikati ya jiji. Kwa idadi ya watu inayokadiriwa kuwa takriban milioni 4.5 ndani ya jiji na zaidi ya milioni 10 katika eneo la mji mkuu(Metro), Nairobi ni kitovu kikuu cha uchumi katika Afrika Mashariki. Inahudumu kama kituo muhimu cha kifedha, biashara, na usafiri, ikiwa na makao makuu ya mashirika mengi ya kimataifa, kampuni za kimataifa, na mashirika ya Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa(UNEP).

Ukweli wa haraka Jiji ...
Thumb
Sanamu ya Jomo Kenyatta.


Lugha zote za Kenya huzungumzwa Nairobi, lakini hasa ni Kiingereza na Kiswahili pamoja na Sheng.

Remove ads

Eneo la jiji la Nairobi

Thumb
Kaunti ya Nairobi (nyekundu) ndani ya jiji kuu la Nairobi (kijani).

Nairobi yenyewe iko ndani ya eneo la jiji la Nairobi (kwa Kiingereza: Greater Nairobi Metropolitan region) lililoundwa na kaunti 4 kati ya jumla ya 47 za Kenya.

Kaunti hizo ni:

Maelezo zaidi Eneo, Kaunti ...

Source: Kenya Census

Eneo hilo linazalisha asilimia 60 za pato la taifa.

Remove ads

Mazingira na hali ya hewa

Nairobi iko kilomita 150 upande wa kusini ya ikweta kwenye nyanda za juu za Kenya kando la mto Nairobi. Nairobi imeanzishwa mahali ambako nchi tambarare ya mto Athi inaanza kupanda juu hadi milima ya Ngong na vilima vingina vinyvyofanya ukuta wa mashariki wa Bonde la Ufa.

Kitovu cha Nairobi kiko zipatao m 1624 juu ya UB. Sehemu za mashariki za jiji ziko bado kwenye tambarare, na sehemu za magharibi ziko kwenye mtelemko unaopanda hadi mita 1800 kwenye mpaka wa jiji na mita 2000 juu ya UB kwenye nje ya jiji huko Limuru.

Hali ya hewa haina joto kali. Halijoto ya wastani ni 20,5°C mwezi wa Machi, na 16,8°C mwezi wa Julai. Wakati wa Juni na Julai usiku unaweza kuwa baridi halijoto ikishuka chini ya sentigredi 10.

Mvua nyingi hunyesha mwezi Machi (mm 199), kiangazi kina mm 14 tu wakati wa Julai.

Remove ads

Historia

Chanzo kwenye kambi la reli

Nairobi ilianzishwa na Waingereza mwaka 1899 kama kambi ya kujenga Reli ya Uganda. Njia ya reli ilikuwa imefika kutoka Mombasa ikaonekana ya kwamba kuanzia hapa kasi ya ujenzi itachelewa kutokana na ugumo na eneo la Bonde la Ufa na mitelemko yake mikali. Mahali palikuwa karibu katikati ya Mombasa na Kampala, palikuwa na maji pakaonekana panafaa kwa kituo njiani. Hasahasa ilionekana tabianchi ya nyanda za juu ilifaa kiafya kwa Waingereza walioteswa na joto la pwani na kwenye nyanda za chini.

Kitangulizi cha Nairobi kilikuwa kituo kidogo kilichoanzishwa mwaka 1896 kando ya mto Nairobi na wakala Mwingereza wa reli kwa kusudi la kuajiri wafanyakazi wazalendo kwa ujenzi wa reli. Mwaka uliofuata 1897 wakaguzi walioandaa njia ya reli walipiga kambi karibu naye. [2].

Mji mkuu wa koloni

Njia ya reli ilifika kwenye kambi tarehe 30 Mei 1899. Hapo idadi ya wafanyakazi - hasa Wahindi - iliongezeka sana na kambi lilikuwa kubwa ya mahema na ghala za vifaa vya ujenzi. Mwezi wa Juni mizigo ya mabati ilifika kutoka Mombasa - tayari kwa reli - na majengo ya kudumu yalianza kutengenezwa katika mazingira ya eneo la kituo cha reli cha leo. Mwezi wa Agosti kamishna Mwingereza wa jimbo la Ukamba[3] aliamuliwa kuhamisha makao makuu yake Nairobi kutoka Machakos akajenga boma lake kwenye eneo la Moi Avenue, mbali na reli jinsi inavyoonekana hadi leo kwenye majengo ya polisi ya kihistoria yanayotazama Bustani ya Jivanji[4].

Barabara kuu ya kwanza ilikuwa "Station Road" [5] kandokando ya Mtaa wa Tom Mboya wa leo iliyoitwa Victoria Street ikawa mahali pa maduka na hoteli za kwanza zilizoendeshwa na Wazungu na baadaye pia na Wahindi kadhaa. Soko la Wahindi maskini likuwa kando. Kwenye sehemu kati ya mitaa ya Haile Selassie na Harambee kulikuwa na makazi ya kwanza ya wafanyakazi. Mwaka uleule wa 1899 ofisi kuu ya reli ikapelekwa huko kutoka Mombasa kwa shabaha ya kurahisisha mawasiliano.

Pale mwanzoni kulikuwa na wasiwasi kuhusu chaguo la mahali; baada ya mvua kali sehemu ya mahema na vibanda vilipatikana katikati ya ziwa la matope. Magonjwa yalisambaa na baada ya epidemia ya tauni soko la Wahindi Lilichomwa na kuhamishwa sehemu nyingine. Majaribio ya kukausha kinamasi yaliendelea kwa miaka kadhaa hadi kufaulu. Kutokana na usumbufu wa matope maafisa wa ngazi ya juu walijenga nyumba zao kwenye kilima cha karibu kilichojulikana kama Nairobi Hill.

Mwaka 1905 Waingereza walihamisha ofisi kuu ya serikali yao ya kikoloni kutoka Mombasa kwenda Nairobi, ambayo ikawa hivyo makao makuu ya Afrika ya Mashariki ya Kiingereza (British East Africa, baadaye Kenya Colony).

Uchumi wa mji ulitegemea pale mwanzoni hasahasa mahitaji ya utawala wa serikali na reli na utalii; matajiri wengi kutoka pande zote za dunia waliFIka kwa kusudi la kuwinda wanyama wakubwa [6] wakivutwa na wingi wa wanyama kwenye nyanda za juu na usafiri rahisi kwa reli. Baadaye ardhi katika mazingira ya mji ilitolewa kwa walowezi Wazungu na kilimo cha biashara kilianza kuchangia.

Kiasili Nairobi ilikuwa imepangwa kwa ajili ya Wazungu wa reli na serikali pamoja na Wahindi; Waafrika hawakupewa makazi isipokuwa mabweni ya wanfanyakazi wa reli na vibanda vya wafanyakazi wasaidizi kandokando ya nyumba za mabwana wao.

Lakini Waingereza waliajiri askari kutoka Sudan na Somalia katika jeshi na polisi, na hao walifuatwa na wafanyabiashara kutoka kwao. Wapagazi na askari kutoka sehemu mbalimbali za Afrika ya Mashariki walifika Nairobi kikazi na wengine waliamua kubaki. Mitaa ya vibanda iliota haraka nje ya mji wenyewe, mingine ilibomolewa haraka, mingine iliweza kubaki. Mnamo 1921 kulikuwa na Waafrika 12,000 waliokaa katika mitaa ya Waafrika iliyoitwa Mombasa, Masikini, Kaburini, Kariokor, Kibera, Pumwani na Pangani.

Tangu uhuru

Mwaka 1963 ikawa mji mkuu wa nchi huru ya Kenya ikaendelea kukua haraka.

Remove ads

Nairobi ya leo

Thumb
Nairobi leo: New Central Bank Tower (140 m), Teleposta Towers (120 m), Kenyatta International Conference Centre (105 m), NSSF Building (103 m), I&M Bank Tower (100 m), Government Office Conference Hall (98 m).

Nairobi imeibuka kuwa mmojawapo kati ya miji mikubwa katika bara la Afrika. Mashirika mengi makubwa duniani yamefungua ofisi zao zinazoshuhudia eneo la Afrika ya Mashariki na Afrika ya Kati. Mojawapo ya mashirika haya ni ofisi za tawi la Umoja wa Mataifa (United Nations), UNEP. Kunazo pia ofisi za mabalozi wa nchi mbalimbali duniani.

Nairobi, kama miji mingi mikubwa, ina matatizo mengi yanayotokea kwa sababu ya ukubwa wake. Watamaduni walioupanga mji wa Nairobi hawakutegemea kuwa utatanuka hivyo. Wataalamu wengi wametoa maonyo mengi kuhusu ukubwa wa mji huu na uwezo wake wa kuwahudumia wakazi wote ambao wanazidi kuongezeka kila mwaka.

Nairobi imewavutia wakazi wengi, wote wakiwa na hamu ya kujitafutia riziki yao. Ijapokuwa wapo wanaofanikiwa, wengi wao hujipata wameangulia patupu wakaachwa bila pesa au hali ya kujikimu. Jambo hili limepelekea kuwepo kwa wakazi wa maeneo yasiyotengwa wananchi, maarufu kama 'slums' kwa Kimombo. Eneo kubwa zaidi jijini Nairobi ni Kibera. Eneo hili lina ukubwa wa kilomita 2 kwa 2 na wakazi takribani milioni moja. Eneo hili halina mipango yoyote ya kuruhusu binadamu kuishi lakini umaskini umewavutia wengi kuishi kule.

Kunayo pia matatizo ya ujambazi na utekaji nyara wa magari. Matatizo haya yamesababisha watu wengi kutoupendelea mji wa Nairobi.

Maelezo zaidi Mwaka, Wakazi ...
Thumb
Picha ya Nairobi kutoka Westlands

Maeneo bunge

Thumb
Kenyatta International Convention Centre na Times Tower.

Kaunti ya Nairobi imegawanywa katika maeneo bunge 17 na kata 85,[7].

Maelezo zaidi Maeneo bunge, Kata ...
Remove ads

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads