Bahama
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Bahama au Visiwa vya Bahama ni nchi ya visiwani katika bahari ya Atlantiki, kaskazini kwa Kuba na mashariki kwa Florida (Marekani). Visiwa hivyo 700 na zaidi viko nje ya Bahari ya Karibi lakini mara nyingi huhesabiwa kati ya Visiwa vya Karibi. Visiwa vingine vya funguvisiwa hilo viko chini ya Uingereza hata leo (Turks na Caicos).Mji mkuu wa Nassau uko kwenye kisiwa cha New Providence.
Remove ads

Inaaminiwa ya kwamba mahali pa kwanza pa Amerika alipofika Kristoforo Kolumbus kilikuwa kisiwa kimoja cha Bahamas, labda San Salvador.
Remove ads
Watu
Wakazi walio wengi (90.6%) wana asili ya Afrika lakini wanatumia lugha ya Kiingereza. Wazungu ni 4.7%.
Upande wa dini, unaongoza Ukristo wa madhehebu mbalimbali (93%), kuanzia Wabaptisti (35%), Waanglikana (15%), Wakatoliki (14.5%), Wapentekoste (13%), Wasabato (5%), Wamethodisti (4%) n.k.
Tazama pia
Viungo vya Nje
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Bahama kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads