Pakistani

From Wikipedia, the free encyclopedia

Pakistani
Remove ads

Pakistani ni nchi ya Asia ya Kusini. Imepakana na Ghuba ya Uarabuni upande wa kusini, Afuganistani na Uajemi upande wa magharibi, Uhindi upande wa mashariki na Uchina kaskazini-mashariki.

Ukweli wa haraka
Remove ads


Thumb
Ramani ya Pakistan

Mipaka yake na Uhindi na Uchina haitambuliki kimataifa. Pakistan na Uhindi zote mbili zinadai eneo la Kashmir zikitawala kila moja sehemu za eneo hili.

Jina la Pākistān lina maana ya "nchi ya watu safi" kwa Kiurdu.

Pakistani ina nafasi ya sita kati ya nchi duniani zenye watu wengi.

Ni nchi yenye Waislamu wengi duniani baada ya Indonesia.

Remove ads

Historia

Wakati wa ukoloni

Pakistani ilikuwa sehemu ya Uhindi wa Kiingereza hadi 1947.

Mwaka 1857 Wahindi walipinga utawala wa Kampuni ya Kiingereza kwa Uhindi wa Mashariki. Matokeo yake utawala ulishikwa na serikali yenyewe ya Uingereza kama koloni (1858).

Mwisho wa karne ya 19 harakati za Wahindi kutafuta uhuru zilianza upya. Mwaka 1885 chama cha INC (Indian National Congress) kiliundwa na Wahindu na Waislamu pamoja waliodai uhuru.

Mwaka 1906 viongozi Waislamu walitoka katika INC na kuunda "Shirikisho la Waislamu".

Mwaka 1917 Uingereza ulitamka ya kwamba ulitaka kuelekea polepole hali ya kujitawala kwa Wahindi. Viongozi wa wenyeji hawakuridhika na mkasi wa mabadiliko. Chini ya uongozi wa Mahatma Ghandi mwendo wa kupigania uhuru bila mabavu ulipata nguvu. Ghandi alipigania hasa umoja wa Wahindu na Waislamu lakini alipingwa na viongozi wenye itikadi kali wa pande zote mbili.

Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia Waingereza walikubali kujiondoa katika Uhindi. Swali kubwa lilikuwa kama nchi itabaki kama nchi moja au kama maeneo ya Waislamu yatajitenga.

Baada ya uhuru

Tarehe 14/15 Agosti 1947 utawala wa Uingereza ulikwisha. Bara Hindi iligawanywa katika nchi mbili za Uhindi na Pakistan. Mgawanyo wa Uhindi ulikuja na vita na kumwaga kwa damu nyingi.

Tarehe 30 Januari 1948 Ghandi mwenyewe aliuawa na Hindu mkali aliyemchukia kwa sababu alitaka usawa wa Waislamu na Wahindu.

Wakati ule ilikuwa nchi moja pamoja na Bangla Desh ya leo, lakini mwaka 1971 hizo pande mbili zilitengana baada ya vita kati yao.

Remove ads

Utawala

Nchi ni shirikisho la majimbo manne ya Punjab, Sindh, Jimbo la mpaka wa kaskazini-magharibi na Baluchistan, mbali ya maeneo matatu.

Watu

Lugha rasmi nchini Pakistan ni Kiurdu na Kiingereza. Lugha nyingine ni zaidi ya 60, lakini ni ndogo, zenye wasemaji wachache; karibu zote ni lugha za Kihindi-Kiulaya (angalia orodha ya lugha za Pakistan). Robo tatu za wakazi wanaelewa Kiurdu.

Asilimia 96.4 za wakazi ni Waislamu, hasa Wasuni. Ndiyo dini rasmi. Wahindu ni 2.14% na Wakristo 1.27%.

Ukweli wa haraka National animal, National bird ...

Tazama pia

Marejeo

Loading content...

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads