Bari

From Wikipedia, the free encyclopedia

Bari
Remove ads

Bari (kutoka kigiriki βαρύς: "nzito") ni elementi na metali ya udongo alikalini yenye namba atomia 56 kwenye mfumo radidia ina uzani atomia 137.327. Alama yake ni Ba.


Ukweli wa haraka Bari ...
Thumb
Bari katika chupa ndani ya gesi ya arigoni.
Remove ads

Tabia

Kama metali ya udongo alikalini zote bari humenyuka haraka na haitokei kiasili kama elementi tupu bali katika umbo la kampaundi zake. Ikisafishwa na kutunzwa katika kiowevu cha mafuta au katika angahewa ya gesi adimu ni metali yenye rangi nyeupe-fedha. Hewani inaoksidisha haraka lakini ganda la oksidi halitoshi kuzuia isiwake kutokana na unyevu hewani.

Bari ni sumu kali kwa miili ya wanadamu na wanyama. Lakini kuna pia kampaundi ambazo haziyeyuki kabisa katika maji kama vile sulfati ya bari BaSO4 (inayotokea kama madini kwa jina bariti).

Remove ads

Matumizi

Matumizi yake ni hasa katika teknolojia ya kekee hasa wakati wa kutafuta petroli. Matope ya bariti yateleza yasaidia kuzunguka kirahisi kwa mitambo ya kekee mwambani.

Kuna matumizi mengine kama aloi kwa mfano katika alumini na magnesi. Hutumiwa pia wakati wa kutengeneza vioo vya matumizi ya pekee.

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bari kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads