Elementi za kikemia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Elementi za kikemia ni dutu zenye tabia maalumu zisizotenganishwa kuwa dutu tofauti kwa mbinu za kemia. Elementi tupu ina aina moja tu ya atomi ndani yake.

Dutu na elementi
Kwa mfano maji ni dutu na ndani yake kuna atomi za haidrojeni na oksijeni. Atomi hizo zinashikana kama molekuli. Kwa kuongeza nishati inawezekana kutenganisha haidrojeni na oksijeni kuwa dutu mbili tofauti. Kila moja peke yake haina kitu kingine ndani yake, kwa hiyo ni elementi.
Inawezekana kupasua hata atomi lakini hii si kazi ya kemia bali ni ya fizikia.
Elementi asilia na elementi sintetiki
Kwa jumla kuna elementi 116 zinazojulikana katika Kemia zimo katika jedwali la elementi linaloitwa pia "mfumo radidia".
Kati ya hizo 116 ni 90 tu zinazopatikana kiasili. Nyingine zinatengenezwa katika maabara na hazidumu sana. Katika hizo elementi sintetiki, nyingine zinakaa muda mfupi wa sekunde lakini nyingine zinakaa miaka.
Alama na hali maada
Kila elementi ina alama yake ya kikemia jinsi inavyoonekana katika jedwali la elementi.
Elementi zinatokea kwa hali maada tofauti. Duniani kuna hali za mango, kiowevu na gesi. Penye joto kali kama katika jua kuna pia hali ya utegili (plasma). Mara nyingi elementi zinapatikana katika hali ya kampaundi yaani zimeunganika na elementi nyingine.
Orodha ya elementi
Orodha ifuatayo inataja elementi za kikemia katika mfumo radidia kufuatana na herufi za alfabeti.
Remove ads
Tazama pia
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Elementi za kikemia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads