Basili Mzee
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Basili Mzee (alifariki Kaisarea ya Kapadokia karne ya 4) alikuwa mtoto wa Makrina Mzee, halafu mhubiri maarufu huko Caesarea Mazaca[1]. Yeye na mke wake Emelia wa Kaisarea walijulikana kwa imani yao[2] iliyowafanya wafukuziwe jangwani wakati wa dhuluma ya kaisari Maximian[3].
Familia yao ilikuwa na watoto 10, waliosaidiwa malezi na bibi yao, Makrina Mzee. Babu yao alikuwa mfiadini. Wote wawili wanaheshimiwa kama watakatifu, kama vile Basili Mkuu na watoto wao wengine 4: Makrina Kijana aliyekuwa mmonaki, Petro wa Sebaste aliyekuwa askofu na mwanateolojia huko Armenia, Naukratio aliyekuwa mkaapweke, na Gregori wa Nisa ambaye alifanywa na Basili kuwa askofu wa Nisa|mji huo akaandika vitabu bora kuhusu teolojia na maisha ya Kiroho[4][5].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu[6].
Sikukuu yake huadhimishwa hasa tarehe 30 Mei pamoja na mke wake [7].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads