Bendera ya Polandi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Bendera ya Polandi
Remove ads

Bendera ya Polandi ni ya milia miwili ya kulala yenye rangi za nyeupe na nyekundu. Mlia mweupe uko upande wa juu, mlia mwekundu uko chini.

Thumb
Bendera ya Polandi
Thumb
Bendera ya Polandi pamoja na nembo la kitaifa

Bendera ilianzishwa kwa azimio la Bunge la Polandi mwaka 1831. Rangi hizi mbili zilipatikana katika nembo ya nchi tangu karne tisa ikionyesha tai nyeupe juu ya rangi nyekundu.

Bendera za kufanana

Bendera ileile inapatikana Bohemia (ni sehemu ya Uceki), Thuringia (jimbo la Ujerumani) na Kantabria (jimbo la Hispania). Bendera zinazofanana ziko Monako, Indonesia na Solothurn (jimbo la Uswisi) (rangi zilezile lakini mlia mwekundu uko juu).

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads