Indonesia

From Wikipedia, the free encyclopedia

Indonesia
Remove ads

Indonesia ni nchi za visiwa katika Asia ya Kusini-Mashariki. Iko upande wa Kusini-Mashariki kati ya Bahari ya Hindi na Pasifiki. Visiwa vyake ni sehemu ya Funguvisiwa la Malay, ingawa Guinea Mpya kwa kawaida haihesabiwi katika fungu hilo. Indonesia imepakana na Papua Guinea Mpya kwenye kisiwa cha Guinea Mpya, pia na Timor ya Mashariki kwenye kisiwa cha Timor, halafu na Malaysia kwenye kisiwa cha Borneo. Nchi nyingine zilizo karibu ni Australia, Singapuri na Ufilipino.

Ukweli wa haraka Jamhuri ya Indonesia Republik Indonesia (Kiindonesia), Mji mkuu na mkubwa ...

Indonesia ni taifa lenye wakazi wengi wa Kiislamu duniani, likiwa na idadi ya watu inayozidi milioni 270, na hivyo kuifanya kuwa nchi ya nne kwa idadi ya watu duniani. Mji mkuu wake ni Jakarta, jiji kubwa lenye shughuli nyingi za kisiasa, kiuchumi na kitamaduni. Lugha rasmi ni Kiindonesia (Bahasa Indonesia): ingawa kuna zaidi ya lugha 700 zinazozungumzwa nchini humo, lugha hiyo inatumika kama chombo cha kuunganisha wananchi wa makabila mbalimbali.

Historia ya Indonesia imeathiriwa na mchanganyiko wa dini, biashara na ukoloni. Kabla ya ukoloni, Indonesia ilikuwa nyumbani kwa falme mbalimbali zenye ushawishi mkubwa kama vile Srivijaya na Majapahit. Katika karne ya 16, Wareno na baadaye Waholanzi walifika na kudhibiti maeneo mengi, hasa kupitia Kampuni ya Kiholanzi ya India ya Mashariki. Indonesia ilijipatia uhuru kutoka kwa Uholanzi mwaka 1945 chini ya uongozi wa Sukarno. Tangu wakati huo, nchi imepitia vipindi mbalimbali vya kisiasa, ikiwa ni pamoja na utawala wa kijeshi, hadi kuanzishwa kwa demokrasia ya kisasa mwishoni mwa karne ya 20.

Remove ads

Jiografia

Indonesia ni nchi ya visiwa 18,000 ilhali zaidi ya 6,000 kati ya hivyo vinakaliwa na watu.

Visiwa vikubwa vyenye wakazi wengi ni hasa vitano:

Historia

Visiwa vya Indonesia viliathiriwa na utamaduni wa Uhindi. Kisiasa kulikuwa na falme nyingi.

Tangu karne ya 17 Waholanzi walianza kujenga vituo na kueneza utawala wao. Waliita koloni lao "Uhindi wa Kiholanzi" ("Nederlands-Indie").

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia Japani ikatwaa visiwa na kuwafukuza Waholanzi.

Mwisho wa vita kiongozi Sukarno akatangaza Indonesia kama nchi huru. Waholanzi walijaribu kurudisha utawala wao lakini walilazimishwa na Marekani kukubali uhuru wa nchi.

Remove ads

Demografia

Nchi ina wakazi 270,203,917 (2020) hivyo ina nafasi ya nne kati ya mataifa makubwa duniani. Ni nchi yenye Waislamu wengi kuliko nyingine zote duniani. Makabila asili ni 300 hivi; kubwa zaidi ni Wajava (42 %).

Lugha rasmi ni Bahasa Indonesia (Kiindonesia) iliyoundwa katika karne ya 20 kama lugha ya taifa kutokana na lahaja ya Kimalay. Nchini kote kuna lugha za asili zaidi ya 700 (angalia orodha ya lugha za Indonesia). Jawa pia ina sanaa ya mwandiko wa kipekee maarufu kama mwandiko wa Batiki (Batik Tulus) unaochorwa kwa jora za nguo.[1]

Idadi kubwa ya wakazi (87.2 %) wanahesabiwa kuwa Waislamu (karibu wote Wasuni), 9.8 % kama Wakristo (Waprotestanti 6.9 %, Wakatoliki 2.9 %), 1.6 % kama Wahindu (hasa kwenye kisiwa cha Bali) na 0.7 % kama Wabuddha. Hizo zote ni dini zilizotambulika rasmi pamoja na ile ya Konfusio (0.05 %).

Mandhari

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads