Brahmagupta
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Brahmagupta (Kisanskrit: ब्रह्मगुप्त)) (597–668 BK) alikuwa Mhindi mtaalamu wa Hisabati na astronomia anayekumbukwa kwa maandishi yake kuhusu fani hizo mbili.

Alikuwa msimamizi wa paoneaanga mjini Ujjain (Madhya Pradesh).
Brahmagupta alikuwa mwanahisabati wa kwanza anayejulikana kutunga sheria za kupiga hesabu kwa kutumia sifuri. Alitunga pia sheria za hesabu kwa namba hasi.
Katika fani ya astronomia alipinga mafundisho ya siku zake kuwa dunia ni tambarare akasisitiza ni tufe. Pia alipinga mafundisho kuwa mwezi uko mbali kuliko jua akaonyesha kuwa sharti mwezi uwe karibu zaidi.
Remove ads
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads