Choo cha shimo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Choo cha shimo au choo cha zamani ni aina ya choo ambapo kinyesi cha binadamu hukusanywa kwenye shimo ardhini.

Ufasili na manufaa
Vyoo hivi havitumii maji au hutumia kati ya lita moja na tatu kwa kila mara ya utumiaji kwa vyoo vya shimo vinavyotumia maji ya kumwangwa.[2] Vikijengwa na kudumishwa vyema, vinaweza kupunguza kuenea kwa magonjwa kwa kupunguza kiasi cha kinyesi cha binadamu kwenye mazingira kutokana na kwenda choo mahali wazi.[3][4] Hii hupungza usambazaji wa vimelea kutoka kwa kinyesi hadi chakula unaosababishwa na nzi.[3] Vimelea hivi ni visababishi vikuu vya maambukizi ya kuharisha na maambukizi wa minyoo ya utumbo.[4] Maambukizi ya kuharisha yalisababisha takriban vifo milioni 0.7 vya watoto wa umri wa chini ya miaka mitano mwaka wa 2011 na watoto milioni 250 walikosa kwenda shuleni siku kadhaa.[4][5] Vyoo vya mashimo ni mbinu ya gharama ya chini zaidi ya kuhakikisha kinyesi kimeondolewa karibu na watu.[3]
Remove ads
Ujenzi na uondoaji kinyesi
Kwa kijumla, choo cha shimo huwa na sehemu tatu: shimo la ardhini, sakafu iliyo na shimo dogo, na chumba kilicho na paa.[2] Kwa kawaida, shimo la ardhini huwa na kina cha angalau mita 3 (futi 10 ) na upana wa mita 1 (futi 3.2).[2] Shirika la Afya Duniani kinapendekeza vijengwe mbali kidogo na nyumba, kwa kuzingatia masuala ya harufu inayotoka chooni na ufikiaji wa urahisi.[3] Umbali na maji ya ndani ya ardhi na maji ya juu ya ardhi unafaa kuwa mkubwa iwezekanavyo ili kupunguza hatari ya uchafuzi. Shimo la sakafuni halifai kuzidi upana wa sentimita 25 (inchi 9.8) ili watoto wasije wakaanguka humo. Mwangaza haufai kuingia humo ili kuzuia inzi wasiingie. Jambo hili linaweza kuhitaji kutumia kifuniko kwenye shimo la sakafuni ikiwa halitumiki.[3] Choo kikishajaa hadi mita 0.5 (futi 1.6) karibu na sehemu ya juu, kinafaa kuondolewa kinyesi chote au choo kipya kijengwe mahali tofauti.[6] Udhibiti wa maji maji ya kinyesi yaliyoondolewa chooni huwa tata. Kuna hatari za kimazingira na kiafya yasipodhibitiwa vyema.
Remove ads
Uboreshaji
Choo cha shimo cha kawaida kinaweza kuboreshwa kwa njia kadhaa. Njia ya kwanza ni kuweka mfereji wa kuingiza hewa shimoni hadi juu ya mjengo wa choo. Mfereji huu huboresha uzungukaji wa hewa na kupunguza harufu mbaya ya choo. Pia unaweza kupunguza nzi ikiwa sehemu ya juu ya mfereji huu imefunikwa kwa waya (ambayo kwa kawaida huwa imetengenezwa kwa kioo nyuzi). Katika aina hii ya vyoo, si lazima kifuniko kitumike kufunika shimo la sakafuni.[6] Hatua zingine za uboreshaji zinazoweza kutumika ni pamoja na sakafu iliyojengwa kwa njia inayowezesha maji kutiririkia ndani na kuimarisha sehemu ya juu ya sakafu kwa matofali au simiti ili kuongeza uthabiti.[2][6]
Utumizi, Jamii na Utamaduni
Kufikia mwaka wa 2013, vyoo vya shimo vinatumiwa na takriban watu bilioni 1.77.[7] Hii ni hasa katika mataifa yanayostawi na pia maeneo ya mashambani na majagwa. Mwaka wa 2011, takriban watu milioni 2.5 hawakuwa na vyoo vizuri na watu milioni moja walilazimika kwenda choo katika sehem wazi katika mazingira yao.[8] Kaskazini mwa Asia na Mataifa ya Kusini mwa Sahara yalikuwa na ufikiaji duni zaidi wa vyoo.[8] Katika mataifa yanayostawi, gharama ya choo kidogo kwa kawaida ni kati ya dola 25 na 60 za Marekani.[9] Gharama za kuendelea kuviboresha ni kati ya dola 1.5 na 4 za Marekani kwa kila mtu kwa mwaka, ambazo mara nyingi hazitiliwi maanani.[10] Katika baadhi ya sehemu za mashambani mwa India kampeni ya "Hamna Choo, Hamna Ndoa" imetumika kuhamasisha umma kuhusu vyoo kwa kuwahimiza wanawake wakatae kuolewa na mwanaume asiye na choo.[11][12]
Remove ads
References
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads