Kodata

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kodata
Remove ads
Remove ads

Kodata (kutoka lugha ya kisayansi: Chordata) ni kundi kubwa la wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Thumb
Muundo wa kodata (samaki sahili): 1 = uvimbe wa ugwe wa neva ("ubongo"), 2 = notokodi, 3 = ugwe wa neva, 4 = mkia nyuma ya mkungu, 5 = mkungu, 6 = njia ya chakula, 7 = mfumo wa mzunguko, 8 = atriopori, 9 = uwanda kuzunguka koromeo, 10 = ufa wa tamvua, 11 = koromeo, 12 = uwanda wa mdomo, 13 = minyiri, 14 = mdomo, 15 = gonadi (ovari/kende), 16 = jicho sahili, 17 = neva, 18 = mkunjo wa tumbo, 19 = ini sahili

Ugwe unaunganisha neva ambazo ni muhimu kwa mwili kwa jumla na neva za kila sehemu au kiungo zinatoka hapa. Ugwe wa neva unaenda sambamba na mhimili wa seli ambazo ni imara zaidi ama gegedu au mfupa.

Mhimili huu ni chanzo cha uti wa mgongo kwa wanyama wengi wa kundi hili na kiunzi cha mifupa cha ndani ya mwili.

Kodata waliendelea kutoka kwa wanyama wengine kama Arthropoda wenye kiunzi cha nje.

Katika uainishaji wa kisayansi Kodata ni faila ya wanyama (Animalia). Nusufaila yenye spishi nyingi ni Vertebrata. Hapa mhimili wa kati unaendelea kuwa uti wa mgongo.

Samaki, amfibia, reptilia na mamalia ni oda ndani ya vertebrata.

Remove ads

Picha

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kodata kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads