David Hilbert

From Wikipedia, the free encyclopedia

David Hilbert
Remove ads

David Hilbert (1862 - 1943) alikuwa mtaalamu wa hisabati, mantiki na falsafa ya hisabati kutoka nchini Ujerumani. Huhesabiwa kati ya wanahisabati muhimu zaidi ya karne ya 19 na mwanzo wa karne ya 20.

Thumb
David Hilbert, picha ya mwaka 1912.

Alishughulika maswali ya "invariant theory" na ukubalifu wa jiometria. Aliunda hisabati ya nafasi ya mawanda (dimension) nyingi yaani zaidi ya mawanda 2 ya bapa au mawanda 3 ya nafasi ya kawaida. Hilbert na wanafunzi wake waliandaa sehemu kubwa ya hisabati ilyohitajika kwa ajili ya nadharia ya uhusianifu iliyokamilishwa baadaye na Albert Einstein.

Hilbert alizaliwa tar. 23 Januari 1862 mjini Königsberg katika jimbo la Prussia ya Mashariki [1] Alisoma hisabati kwenye chuo Kikuu cha Königsberg, akachukua digrii ya dokta akaendelea kuwa profesa wa hisabati kwanza Königsberg, halafu Göttingen alipokufa tar. 14 Februari 1943.

Remove ads

Viungo vya Nje

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads